Burudani

Wasanii wakubwa wanne kuto hudhuria tuzo za Grammy mwaka huu,sababu ni….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Baadhi ya wasanii wakubwa Marekani watrakosa kuhudhuria tuzo kubwa za muziki za Grammy Mwaka huu. Drake, Kanye West, Justin Bieber, na Frank Ocean hawata kuwepo kwenye tuzo hizi za Grammys.

Frank Ocean aliyetoa album mbili mwaka jana Blonde na Endless hakupeleka kazi zake kwenye kamati ya tuzo hizo.

Frank amekuwa akiponda tuzo hizo na kudai kuwa haziwakilishi watu waliofanya mambo aliyofanya yeye na kutoka alikotoka yeye.

Kanye West anawania tuzo nane kwenye tuzo hizi za Grammy Mwaka Huu huku akiwa ameshinda Greammy 21 toka kuanza kufanya muziki.

Mwezi wa 10 mwaka huu Kanye alisemakama album ya Frank haitakuwepo kwenye tuzo basi hato hudhuria. Drake pia atakuwa kwenye ziara yake ya “Boy Meets World Tour.” na Justin Bieber hata kuwepo.

Tuzo za 59 za Grammy Awards zinafanyika Feb. 12 pakiwa na show za wasanii kama Adele, Bruno Mars, na John Legend.

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open