Burudani

Love Is a Religion ya Keri Hilson kutoka mwaka huu….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rnb super staa Keri Hilson amekanusha kuwa alitaka kurudi kwenye muziki mwaka jana na kwamba taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari haikuwa kweli.

Mwaka 2016 palikuwa na taarifa iliyosemekana ni rasmi kutoka kwenye Camp ya Keri Hilson ikisema kuna album mpya anatoa mwaka huo na kwamba inaitwa L.I.A.R. (Love Is a Religion).

Keri amesema kwenye kipindi cha The Real kuwa ni kweli album ipo ila haiko tayari kutoka na isingetoka mwaka 2016.Keri pia alipiga chenga swali kuhusu kuachana na mpenzi wake staa wa NBA Serge Ibaka.

Love Is a Religion ni album ya kwanza ya Keri Hilson toka mwaka 2010 alipotoa No Boys Allowed. Ukiacha album mpya, Keri ana comedy kwenye tv iliyopewa jina Love By the 10th Date, inaanza Jan. 28.

Tazama na Sikiliza Interview Za Kuburudisha Kwenye Channel Yetu,Bonyeza HAPA

Weka Comments Hapa

Open