Michezo

PSG Kuchunguzwa na Shirikisho la soka barani Ulaya

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeanza kufanya uchunguzi wa “Financial Fair Play ” katika klabu ya PSG kufuatia matumizi ya klabu hiyo katika dirisha la usajili majira ya kiangazi.

Matajiri hao wa Paris wameweka rekodi ya usajili kwa kumnunua Neymar Jr kutoka Barcelona kwa pauni milioni 198 na kumchukua Kylian Mbappe kwa mkopo kutoka Monaco na kukubaliana kutoa pauni milioni 166 ili kumsajili moja kwa moja Mfaransa huyo mwisho wa msimu huu.

Sheria ya Financial Fair Play (FFP) ililetwa katika soka la Ulaya ikiwa na nia ya kutaka klabu kuweka Uwiano, Mizani au Uhalali wa matumizi yao na mapato yao.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open