Burudani

Rapa Big Sean amsaliti Jhene Aiko na Nicole Scherzinger

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Msanii wa Soul, Rnb na Pop Jhene Aiko anaweza kuwa miongoni mwa wanawake maarufu wenye bahati mbaya sana na wanaume kwenye maisha yake.

Ikiwa ni miezi michache imepita toka ametengana na mume wake, Jhene Aiko aliweka wazi kuwa alikuwa na Big Sean baada tu ya kuachana na mume wake na sasa Big Sean amemsaliti.

Big Sean anaripotiwa kulala na aliyekuwa msanii wa kundi la The Pussycat Dolls, Nicole Scherzinger baada ya tuzo za Oscars, Jhene Aiko alifanya ku unfollow kurasa ya instagram ya Big Sean na kuzua tetesi za kuachana.

Big Sean na Nicole walikuwa wakionyesha kupendana na kutakana sana kwenye After party ya tuzo za Oscar na taarifa hizi alifikishiwa Jhene Aiko.

Aiko alikuwa na Big Sean toka 2016 kabla ya kuachana rasmi na mume wake Dot Da Genius, Aiko ana mtoto na kaka yake Omarion ‘O’Ryan’, Big Sean aliwahi kuwa na mahusiano na mastaa kama Ariana Grande na mwigizaji Naya Rivera.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open