Burudani

Trailer ya filamu ya maisha ya Oscar Pistorius na alivyompiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp,familia yake ilichosema

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Familia ya mwanariadha mlemavu wa miguu kutoka nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyefungwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp imetoa tamko lenye nia ya kwenda mahakamani kuzuia kutolewa kwa filamu inayohusu maisha ya mtoto wao Oscar Pistorius.

Filamu hiyo iliyopewa jina Blade Runner Killer inatarajiwa kutoka Marekani mwezi wa kumi na moja mwaka huu.

Kwa upande wa familia ya Familia ya mwanariadha huyo wanasema kwamba huo ni uwazi mbaya kabisa wa ukweli kuhusu mtoto wao

Nayo familia ya marehemu Steenkamp imesema hadithi ama maudhui ya filamu hii ni kutokana na mtazamo wa Reeva na mama yake.

Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela mwaka 2016 baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open