Burudani

Producer Rick Rubin asema Eminem anakerwa na mtindo wa RAP wa kumumunya maneno

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Baada ya kutoa colabo yake na Beyonce ‘Walk On Water’ staa wa hiphop Eminem ameongea na producer maarufu wa hiphop Rick Rubin na mwandishi Malcolm Gladwell katika Episode ya kwanza ya “Broken Record,”.

Kwenye mazungumzo yao Rick Rubin anasema Amegundua kuwa Eminem amechoshwa kabisa na mtindo mpya ya kurap kwa kumeza Meza na kumumunya maneno, “Mumble Rap”.

Eminem kama mwanafunzi wa HipHop huwa anasifia  muziki uliofanywa na wasanii kama Tupac Shakur, Ice-T, N.W.A, Kool G Rap, Big Daddy Kane, Masta Ace, JAY-Z, AZ, Nas, Wu-Tang Clan, Big L, na The Notorious B.I.G ila hivi karibuni ameonyesha kuchukizwa na mtindo unaofanywa na wasanii wengi wa rapa kama MIGOS na Young Thug.

Wimbo wa “Walk On Water” utasikika kwenye album mpya ya Eminem Revival.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open