Burudani

Stori, kabla ya kifo chake dictator Saddam Hussein alimsikiliza zaidi Mary J Blige na muziki wa Hiphop…

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein alitumia siku zake za mwisho duniani kusikiliza muziki wa hiphop na muziki wa msanii Mary J Blige.

Hii ni kwa mujibu wa kitabu kipya kuhusu maisha yake kilichoandikwa na mwanajeshi Will Bardenwerper The Prisoner in His Palace: Saddam Hussein, His American Guards, and What History Leaves Unsaid.

Kitabu hichi kinasema wanajeshi waliomlinda Saddam walijikuta wanakuwa marafiki zake wakati akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na jeshi la Marekani.

Saddam alipenda show za tv za Marekani kama Sesame Street na filamu kama Dracula, Saddam pia alipenda sana kusikiliza muziki wa HipHop hususan muziki wa Mary J Blige.

Vitu vingine alivyopenda ni pamoja na sigara za Cohiba na kuendesha basikeli, kitabu hichi kinatoka mwezi huu wa sita 2017.

Hapa ndipo alipolala Saddam Hussein kwa miaka mitatu

#SammisagoNEWS

 

Weka Comments Hapa

Open