Burudani

Msanii Sean Kingston ametangaza kufilisika na kwamba kwa sasa anaishi na Mama yake…

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Hit Maker wa “Beautiful Girls” Sean Kingston ametangaza kufilisika na kwamba kwa sasa anaishi na mama yake.

Sean Kingston ametoa kauli hii baada ya kushindwa kulipa pesa anazodaiwa na wakili wake ambazo ni dola za kimarekani 12500, Tanzania ni zaidi ya milioni 24.

Sean anasema kwenye akaunti yake ya benki ana dola $500 tu ambazo ni kama milioni 1 ya Tanzania

Mwaka 2015, wakili James J. Gangitano alifungua mashtaka dhidi ya Kingston, kwa kushindwa kumlipa pesa zake na Sean aliahidi kumlipa January mwaka huu.

Baada ya kufunguliwa kesi ya madai na wakili wake, Sean Kingston ameamua kujaza form ya kufilisika akionyesha kwa sasa hana umiliki wa mali yoyote , anaishi na mama yake Janice Turner mjini Los Angeles.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open