Burudani

Suge Knight asema hana imani kuwa 2 Pac amekufa

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako
Kwenye Interview ndefu itakayoruka weekend hii nchini Marekani ikiwa na ushahidi mpya kuhusu kifo cha 2 Pac, mmiliki wa Death Row Records Suge Knight amesema hana uhakika kama 2 Pac amekufa.
Suge ambaye alikuwa kwenye gari wakati 2 Pac anapigwa risasi amesema kwenye interview na Ice T na mwandishi Soledad O’Brien “Nilipoondoka Hospitalini baada ya 2 Pac kuhudumiwa kutokana na kupigwa risasi, alikuwa powa tu na tulitaniana na kucheka, Sioni jinsi gani mtu anaweza badilika hali kutoka kuwa na nafuu mpaka kuwa na hali mbaya kabisa”
Akaulizwa Je 2 Pac Yuko hai, alijibu> Nakwambia, Jinsi alivyo 2 Pac, huwezi kujua. 
Interview hii inaitwa “Who Shot Biggie & Tupac?” itaruka Jumapili hii ikiongelea mauwaji ya wasanii wakubwa wa hiphop Christopher “The Notorious B.I.G.” Wallace na 2Pac.
Shakur alifariki Sept. 13, 1996 baada ya kupigwa risasi mjini Las Vegas na Wallace alifariki March 9, 1997 baada ya kupigwa risasi mjini Los Angeles.
Waliofanya mauwaji haya hawajawahi kukamatwa.
#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open