Burudani

Baada ya miaka mitano T-Pain yuko tayari kurudi kwenye kiti chake

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

 

Rapa, Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki T-Pain ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya OBLIVION ikiwa ni album ya kwanza toka mwaka 2011 alipotoa ‘REVOLVER’.

Teddy P aka T-Pain amesema album mpya OBLIVION inatoka November 17, single zlizotoka ni pamoja na “Goal Line” Ft Blac Youngsta na “F.B.G.M.” Ft Young M.A.

T-Pain alipotea kwenye muziki mwaka 2014 baada ya msongo wa mawazo kuhusu kupondwa na kejeli zilizokuwa zikimzunguka wakati anatumia AUTO TUNE kufanya sauti yake ipendeze zaidi kwenye muziki wake, mwaka huo huo T Pain alisema kwenye interview kuwa dili lake la kujiunga na Young Money lilishindwa kukamilika sababu mabosi wa lebo za Cash Money na Young Money Baby, Lil Wayne, Slim waliamini yeye ni mlevi zaidi na atakuwa hasara kwao.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open