Burudani

Fergie kujitoa kwenye kundi la The Black Eyed Peas,nafasi yake itachukuliwa na….

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

First Lady wa kundi la The Black Eyed Peas ‘Fergie’ ameripotiwa kujitoa kwenye kundi hilo ili kufanya kazi zake kama msanii huru, nafasi yake itachukuliwa na Nicole Scherzinger.

Msemaji wa The Black Eyed Peas, Will.i.am ameongea na jarida la Emirati Ahlan! nakusema “Kwa sasa hakuna mtu anachukua nafasi ya Fergie kwenye kundi la The Black Eyed Peas, tuko kwenye ziara ya kusheherekea miaka 20 ya kundi, yeye anarekodi kazi zake binafsi, tuna album yetu mpya inaitwa Masters Of The Sun na humu atasikika Nicole Scherzinger wa Pussycat Dolls“.

Kauli ya Will.i.am imethibitisha kuwa badala ya Fergie kusikika kwenye album hii, atasikika zaidi staa Nicole Scherzinger wa The Pussy Cat Dolls.

Variety iliripoti wiki iliyopita kuwa Fergie atajiunga na lebo mpya ya BMG, na kufanya nayo kazi pamoja na lebo yake binafsi ya Dutchess Music baada ya kujitoa Interscope Records.

Nicole Scherzinger wa The Pussy Cat Dolls

Fergie

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open