Michezo

Usain Bolt kuanza majaribio ya kucheza soka na klabu ya Borussia Dortmund.

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Nyota wa zamani wa riadha duniani Usain Bolt kutoka Jamaica, amesema amepona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu, na sasa yupo mbioni kufanya majaribio kwenye klabu ya Borussia Dortmund.

Bolt mwenye umri wa miaka 31, amesema mwezi Machi atafanya majaribio ili kujua nini anahitaji kuongeza ili aingie rasmi kwenye soka la ushindani, ambayo ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu, huku akisema lengo lake ni kuichezea klabu anayoishabikia ya Manchester United.

Bolt alisema “Mwezi Machi nitafanya majaribio kwenye klabu ya Dortmund, hatua ambayo itaamua nini cha kufanya ili niwe mchezaji kamili, na wakisema mimi ni mzuri basi nitaanzia hapo kuhakikisha ndoto yangu ya kuchezea Manchester United inatimia”,

Bolt ambaye ni raia wa Jamaica, anahesabiwa kama mwanariadha bora zaidi kuwahi kutokea baada ya kushinda medali za dhabau kwenye michuano nane tofauti ya Olimpiki.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open