Michezo

Wallace Karia ameshinda Urais wa TFF kwa kura 95 kati ya kura 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Rais mpya wa TFF ametangazwa Dodoma, Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.

Rais mpya wa TFF ni Walace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.

Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.

Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.

Matokeo Kamili ya Urais TFF

Emmanuel Kimbe>1

Fredy Mwakalebela>3

Imani Madega>8

Richard Shija>9

Ally Mayai>9

Wallace Karia>95

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open