Burudani

Rapa Lil Wayne alivyotishia kuifuta Young Money kwenye ramani ya muziki na Dunia

By  | 
Share Habari Na Marafiki Zako

Staa mkubwa mwenye ushawishi kwenye Rap na HipHop Lil Wayne ametishia kuifuta kabisa lebo yake ya Young Money kama Cash Money wameshindwa kuisimamia na kuiendesha vizuri.

Lil Wayne amempa jaji malalamiko na mapendekezo yake kuhusu lebo hio kupata mwendeshaji mzuri au kuifuta kabisa kama hatapatikana mtu huyo mapema, na jaji ameombwa kusikiliza malalamiko ya ugawanywaji hisa za lebo hio.

Baada ya jaji kusikiliza upande wa Wayne, alisikiliza upande wa Brian “Birdman” Williams ambaye anaendesha lebo hio chini ya Cash Money, Birdman amesema Lil Wayne hana haki za kufuta lebo hio akiwa chini ya Cash Money, akiwa nje ya Cash Money angeweza kufanya hivyo.

Beef hili la Lil Wayne na Birdman limeanza toka December 2014, Wayne alipoanza kufunguka kuhusu matatizo ya lebo hio.

#SammisagoNEWS

Weka Comments Hapa

Open